Kansela wa Ujerumani Scholz yuko ziarani Japan

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz atakutana leo na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida mjini Tokyo katika ziara yake ya kwanza barani Asia tangu alipoingia madarakani. Scholz, ambaye aliondoka Berlin jana jiioni, atafanya ziara ya siku mbili nchini Japan ambapo anatarajiwa kuhudhuria hafla ya chakula cha jioni itakayoandaliwa na mwenyeji wake na pia kulihutubia jukwaa la kibiashara lililoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda cha Ujerumani nchini Japan. Hata hivyo, huku vita vya Urusi nchini Ukraine vikiendelea kupamba moto, na China ikiendelea kudhihirisha ushawishi wake duniani, masuala ya usalama yanatarajiwa kutawala mada za ziara ya kansela Scholz. Anatarajiwa kusisitiza kuhusu umuhimu unaokuwa wa Japan kwa Ujerumani, na kuwa Berlin haijalifumbia macho bara la Asia, licha ya changamoto kubwa barani Ulaya.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii