SERIKALI
imeuelekeza uongozi wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania ambayo inajenga
meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu kuzingatia makubaliano yote
yaliyomo kwenye mkataba wa ujenzi wa meli hiyo.
Kauli hiyo
imetolewa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Mei 14, 2022
katika kikao kati yake na Balozi wa Korea ya Kusini nchini, Kim Sun Pyo
kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es
salaam.
Katika Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa Mkurugenzi
wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania Bw. Kwak ambaye alikiri mapungufu
katika utekelezaji wa mradi huo na aliahidi kuwa kampuni yake itaongeza
kasi ya ujenzi ili ukamilike kwa wakati na meli hiyo iwezo kuwahudumia
wananchi kama ilivyokusudiwa.
Pia, Mheshimiwa Waziri Mkuu
ameelekeza kuwa watalaamu wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania
warejeshewe Pasi zao za kusafiria ambazo zilizuiwa na s
Serikali kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mwenendo wa ujenzi wa meli hiyo.
Kikao
hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika ya Mashariki, Mbarouk Mbarouk na Naibu Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi, Fred Mwakibete.
Wengine ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu
wa Kampuni ya Huduma za meli, Philemon Bagambilana na Kanali Samwel
Mahirane ambaye ni Kamishina wa Uhamiaji, Usimamizi na Udhibiti wa
Mipaka nchini.