Mkenya anayepambana na ukeketaji ametangazwa kuwa muuguzi bora zaidi duniani

Muuguzi wa Kenya ameshinda tuzo ya kwanza kuwahi kuepo ya uuguzi duniani ambayo ina zawadi ya $250,000.

Anna Qabale Duba, ambaye anafanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Marsabit kaskazini mwa Kenya, alitunukiwa kwa kujitolea kutokomeza mila potofu kama vile ya ukeketaji katika jamii yake.

Bi Duba pia ameanzisha taasisi - Qabale Duba Foundation - inayolenga kuwawezesha wasichana wadogo.

"Kupitia shirika langu, nimejenga shule ya kipekee kijijini kwangu inayofundisha watoto na wazazi wao, kwa sababu kwangu elimu ni muhimu kwa maisha bora ya baadaye," Bi Duba alisema katika hotuba yake.

Zaidi ya wauguzi 24,000 kutoka nchi 184 waliwasilisha maombi yao.

Aliadhimishwa huko Dubai katika sherehe iliyofanyika katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wauguzi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii