Serikali ya Marekani imeonya kuhusu uwezekano kwa kutoka kwa shambulio la kigaidi katika eneo la Goma, Mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo sehemu ambao imekuwa ikishuhudia ongezeko la utovu wa usalama kwa miezi kadhaa sasa.
Katika taarifa yake kuhusu hali ya usalama nchini humo, ubalozi wa Marekani jijini Kinshasa, umeelezea uwezekano mkubwa wa kutokea kwa shambulio la kigadi, machafuko, makabiliano ya makundi ya watu wenye silaha pamoja na visa vya utakaji mjini Goma kivu kaskazini.
Kitengo cha usalama cha Marekani katika ubalozi wake jijini Kinshasa kimeeleza kuwa kuna uwezekano wa kutekelezwa kwa shambulio kwa feri itakayokuwa ikitokea Goma japokuwa taarifa ya Marekani haikuweka wazi ni feri ipi inayolengwa.
Washington imewataka polisi nchini DRC kuwa waangalifu zaidi wakionya kuhusu mikusanyiko ya watu pamoja na maandamano wakati huu kukitangazwa uwezekano wa kutokea kwa shambulio,raia wa Mareakani wanaoishi nchini DRC wakiombwa kutofanya safari za kuelekea mjini Goma.
Aprili 8, 2022 watu 6 waliuawa katika shambulio la bomu kwenye kambi ya kijeshi ya katindo karibu na mji wa Goma.
Raia wa mashariki mwa Kongo wamekuwa wakishambuliwa na makundi ya watu wenye silaha, waasi wa ADF na CODECO wakituhumiwa kuhusika na mauawaji hayo wanawake na watoto wakiripotiwa kuathiriki zaidi, maelefu wakiyahama makwao.
Jeshi la (FARDC) nchini DRC kwa ushirikiano na UPDF la Uganda wanaedeleza operesheni ya pamoja mashariki mwa Kongo kama njia moja ya kumaliza mashambulizi ya waasi.