Waliokimbia Ukraine wapindukia milioni 6

Shirika la Umoja wa Mataifa lenye kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema zaidi ya watu milioni 6 hadi sasa wameikimbia Ukraine tangu Urusi ianze uvamizi wake dhidi ya taifa hilo.Kadhalika shirika hilo lenye maskani yake mjini Geneva, Uswisi limesema idadi ya watu wanaorejea nchini humo kwa kipindi kifupi au moja kwa moja imepindukia milioni 1.6, likiangazia takwimu za watu wanaovuka mpakani.Msemaji wa shirika hilo, Mathew Saltmarsh amesema jumla ya watu milioni 2.4, ambao wamelikimbia taifa hilo wameingia katika mataifa yanayolizunguka taifa hilo, ambayo yanachukua idadi kubwa ya wakimbizi.Poland pekee imewaandikisha wakimbizi zaidi ya milioni 3.2. Taifa hilo na mengine ya Umoja wa Ulaya yamefungua mipaka yake na hivyo kufanya kazi ya kupata idadi kamili ya wakimbizi hao kuwa ngumu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii