Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amesema yupo tayari kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Urusi katika kufanikisha makubaliano lakini pasipo masharti.Akizungumza na televisheni ya taifa ya Italia RAI, amesema taifa lake kamwe halitalimbua eneo la Crimea ambalo lilinyakuliwa mwaka 2014, kama sehemu ya Urusi.Aidha kiongozi huyo aliongeza kusema wanataka Urusi iondoke katika ardhi ya Ukraine kwa kuwa ni taifa huru na halipaswi kukaliwa kijeshi na taifa lingine.Amesema kama rais wa Ukraine anapaswa kutafakari hatma ya mahusiano yao na jirani yao Urusi kwa kuwa marais na vizazi vitabadilika lakini mataifa hayo yataendelea kuwepo.