Ujerumani imesema inaweza kuhimili athari za vikwazo vya nishati ya Urusi

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck amesema athari za vikwazo vya Urusi katika sekta ya nishati ya Ujerumani zinaweza kudhibitiwa.Waziri huyo alikuwa akizungumzia uamuzi wa Urusi kuiwekea vizuizi Kampuni yake ya Gazprom na makampuni tanzu yenye kumilikwa na serikali Ujerumani.Waziri huyo ameliambia bunge la Ujerumani kwamba serikali imejiandaa vyema kwa hali hiyo na nyingineyo itakayojitokeza.Mita za ujazo milioni kumi za gesi zilizokuwa zikiingizwa nchini kutoka Urusi kila siku, zinaweza kufidiwa kwa kuagiza kutoka mataifa mengine ambayo mchakato wa jitihada hizo umeanza.Kwa mujibu wa amri iliyotolewa na Rais Vladimir Putin Jumatano iliyopita kampuni ya Gazprom haiwezi tena kufanya biashara na jumla ya mashirika 31 ya Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii