wito umetolewa kwa vijana hapa nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi na kuchangamkia fursa mbalimbali kadri zinavyojitokeza.
wito huo umetolewa na mwenyekiti wa vijana mtaa wa swila na nyambulogoya kata ya nyegezi jijini mwanza bwn: samuel willium wakati akizungumza na jembe habari.
amesema ili kijana uweze kufanikiwa ni lazima kujitoa kwa hali na mali kuwekeza sehemu za kujitengenezea kipato na sio kukaa bila shughuli yeyote.
aidha samweli amewashukuru vijana ndani ya mtaa wake kuendelea kujitoa kushiriki katika mambo mbalimbali ya furaha na huzuni Na kuwaomba vijana katika mitaa mingine kuendelea kutumika vyema katika maeneo wanamoishi.
Na mwisho kama vijana , ameahidi kuendelea kuonyesha ushirikiano kwa uongozi mpya wa balozi aliyechaguliwa ndani ya mtaa huo.