RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU ATOA SHUKRANI KWA WAUGUZI WOTE.

Ikiwa leo ni siku ya wauguzi duniani, Waziri wa Afya ,ummy mwalimu amewashukuru Wauguzi kwa kazi nzuri wanazoendelea kufanya katika kuwahudumia wananchi, huku akitoa wito kwao kuendelea kutimiza wajibu kwa kufuata miongozo, maadili na Sheria za Baraza lao.
Akizungumza  bungeni mjini dodoma katika mkutano wa saba kikao cha 21 ,waziri UMMY, ameweka wazi kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kuajiri watumishi, hususan Wauguzi ili kuwapunguzia mzigo wakati wa kutoa huduma.

kupitia ukurasa wake wa Twitter rais  wa Tanzania samia suluhu hassan ameandika
'Niwatakieni kheri wauguzi wote nchini katika kusherehekea siku ya wauguzi duniani .
watanzania tunathamini sana mchango wenu muhimu katika kulinda afya ya wananchi .
Tunaendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya afya ili kuimarisha mazingira ya utendaji kazi pamoja na masilahi yenu'
Ni ujumbe huo wa rais samia katika siku hii ya wauguzi duniani.
MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI, KITAIFA YAMEADHIMISHWA MKOANI KILIMANJARO NA MGENI RASIMI NI WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA  NA AMBAYE AMEWAKILISHWA Na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum DOROTH GWAJIMA .
KAULI MBIU ya siku ya Wauguzi duniani kwa mwaka huu ni Wauguzi ni sauti inayoongoza, wekeza na heshimu haki za watu kwa maboresho ya huduma za afya kwa wote.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii