Mwanzilishi mwenza aliyestaafu wa Microsoft na mfadhili mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Bill Gates amepimwa na kukutwa na UVIKO-19, na atajitenga hadi atakapopona. Tangazo hilo lilikuja wakati Gates alikuwa akiandaa mpango wake wa kutetea hatua zaidi za kuzuia janga hilo, na kuchapisha kitabu juu ya mada hiyo.
“Nimepima na kukutwa na COVID. Ninakabiliwa na dalili zisizo na nguvu
na ninafuata ushauri wa wataalam kwa kujitenga hadi niwe na afya tena,”
Gates aliandika Jumanne, na kuongeza,"Nina bahati ya kupewa chanjo na kuimarishwana kupata huduma ya kupima na matibabu makubwa".