Zelensky ataka bandari za Ukraine zifunguliwe

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito hatua zichukuliwe kuzifungua bandari nchini mwake kuepusha mzozo wa chakula duniani. Zelensky amesema biashara katika bandari hizo imesimama na kuitaka jumuiya ya kimataifa ichukue hatua za haraka kufikisha mwisho hatua ya Urusi kuzizingira ili kuruhusu usafirishaji wa ngano. Rais huyo alitoa kauli hiyo baada ya kuzungumza na rais wa baraza la Ulaya Charlees Michel ambaye alikuwa akzuru mji wa Odesa, bandari muhimu katika bahari Nyeusi kwa usafirishaji wa mazao ya kilimo ambako makombora yalivurumishwa katika vituo vya kitalii na kuharibu majengo jana Jumatatu. Wizara ya ulinzi ya Ukraine imesema vikosi vya Urusi vikisaidiwa na vifaru na silaha nzito vilikuwa vikifanya operesheni ya uvamizi katika kiwanda cha Azovstal mjini Mariupol, ambako mamia ya wapiganaji wa Ukraine wamenasa kwa miezi kadhaa ya kuzingirwa eneo hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii