Rais
Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kiserikali ya siku mbili
nchini Uganda kuanzia leo Jumanne Mei 10 -11, 2022, kwa mualiko wa Rais
wa nchi hiyo, Yowei Museveni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa
madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha na kudumisha zaidi historia
iliyopo na mahusiano ya kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa kiuchumi
na kijamii kati ya nchi hizo mbili.
Imeeleza kuwa katika ziara
hiyo, wanatarajiwa kujadili kuhusu masuala ya nishati, biashara,
usafiri, maendeleo ya miundombinu pamoja na sekta za afya.
“Hii
itakua ni ziara ya kwanza ya kiserikali nchini kufanywa na Rais Samia
tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani mwezi Machi 2021”
imeeleza taarifa hiyo.