Wanasiasa wa chama cha Democratic nchini Marekani wamekubali kuharakisha msaada zaidi wa dola bilioni 39.8 kwa ajili ya Ukraine na hivyo kuondoa hofu kwamba kuchelewa kwa kura kungevuruga usafirishaji wa silaha za Marekani kwa serikali ya mjini Kyiv. Baraza la wawakilishi la Marekani huenda likaupitisha mpango huo unaovuka kiwango kilichoombwa na rais Joe Biden mwezi uliopita cha dola bilioni 33 katika kura itakayopigwa leo. Baraza la seneti pia limesema liko tayari kuharakisha kuukamilisha mchakato huo.