Rais mpya wa Korea Kusini kuapishwa leo

Rais mpya wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol anaapishwa leo katika sherehe itakayogubikwa na majaribio ya hivi kariuni ya silaha za nyuklia ya Korea Kaskazini. Utawala wa kihafidhina wa rais Yoon unajiandaa kukaribisha sera ya kigeni yenye nguvu zaidi ya nchi hiyo inayoshikilia nafasi ya 10 kiuchumi duniani baada ya sera iliyotumiwa na rais anayeondoka Moon Jae-un wakati wa muhula wake wa miaka mitano madarakani. Hakuna taarifa nyingi zinazofahamika kuhusu hotuba ya rais Yoon itakayofuatiliwa kwa karibu kuona jinsi anavyopanga kuanza muhula wake wa miaka mitano. Watu takriban 40,000 wamealikwa kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwake. Ikulu ya Marekani ilitangaza wiki iliyopita kwamba rais wa Marekani Joe Biden amemtuma Douglas Emhoff, mume wa makamu wa rais Kamala Harris kuongoza ujumbe wa rais unaowajumuisha watu wanane. Japan na China pia zinawatuma wajumbe wa vyeo vya juu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii