Naibu mkuu wa watumishi katika Ikulu ya Urusi, Kremlin, Sergey Kiriyenko amezuru mjini Mariupul, huko Ukraine, ambao kwa kiwango kikubwa unadhibitiwa na Urusi. Kiongozi huyo ambae aliwahi kuwa waziri mkuu, kwa sasa ni mratibu wa siasa za ndani nchini Urusi.Kupitia ukurasa wake wa telegram, kiongozi wa wanaotaka kujitenga katika eneo la Donetsk, Denis Pushilin amesthibitisha ziara hiyo akisema mbali na kuuzuru mji wa bandari, amefika pia katika kiwanda cha chuma cha Ilich.Kiriyenko na Katibu Mkuu wa chama cha Rais Vladimir Putin cha "United Russia", Andrey Turchak, pia waliutembelea mji wa Volnovakha.