Google Wazindua Kituo cha Ukuzaji wa Bidhaa Nairobi Kenya Ambacho ni cha Kwanza Afrika

Mtandao wa Google umezindua kituo cha ukuzaji wa bidhaa jijini Nairobi Kenya ambacho ni cha kwanza katika bara la Afrika ambacho kitakua kikifanya kazi ya kujenga bidhaa na huduma za ‘mabadiliko’ kwa soko la Afrika na dunia ambapo uzinduzi huu umefanyika baada ya kampuni hii ya Marekani October 2021 kutangaza mipango ya kufanya uwekezaji wa dola bilioni 1 katika miaka mitano ijayo.

Google ilisema itaajiri zaidi ya vipaji 100 vya teknolojia ikiwa ni pamoja na Wahandisi wa programu (software), Watafiti na Wabunifu katika miaka miwili ijayo ili kusaidia kutatua changamoto ngumu na za kiufundi kama vile kuboresha matumizi ya simu kwa Watu barani Afrika au kujenga miundombinu ya mtandao inayotegemewa zaidi.

Google inajiunga na orodha ya makampuni makubwa ya kiteknolojia yaliyoanzisha vituo vya uvumbuzi jijini Nairobi Kenya ambapo wiki mbili zilizopita Microsoft nao walizindua kituo cha utafiti na maendeleo jijini Nairobi, vilevile VISA nayo ilitangaza kuanzisha kituo chake cha kwanza cha uvumbuzi ili kuunda suluhu za malipo na biashara pamoja na Washirika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii