Jaji asema uvaaji barakoa kwenye vyombo vya usafiri Marekani ni kinyume cha sheria

Marekani imeondoa sheria ya kuvaa barakoa katika vyombo vyote vya usafiri. Mahakama moja katika jimbo la Florida imesema kwamba sheria hiyo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona ni kinyume cha sheria. Jaji aliyetoa uamuzi huo amesema kwa kutoa amri ya kuvaa barakoa, mamlaka ya afya nchini humo CDC ilivuka mamlaka yake. Wamarekani walikuwa wanatakiwa kuvaa barakoa wanapokuwa katika ndege, treni na mabasi. Amri hiyo ilikuwa imeongezwa hadi mwezi ujao wa Mei. Ikulu ya White House na wizara ya haki zinaweza kukata rufaa kutokana na uamuzi huo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii