Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Korea Kaskazini Sung Kim amewasili mjini Seoul leo kwa mazungumzo na maafisa wa Korea Kusini juu ya kushughulikia kuongezeka kwa majaribio ya makombora kutoka Korea Kaskazini.Bw Sung ambaye anafuatana na naibu wake Jung Pak katika ziara hiyo ya siku tano atakutana na viongozi wa Korea Kusini akiwemo mjumbe maalumu wa nchi hiyo kuhusu masuala ya nyuklia Noh Kyu-duk.Marekani na mshirika wake Korea Kusini zina wasiwasi na idadi inayoongezeka ya majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini ambayo yamezusha hofu kwamba Pyongyang huenda inataka kuanza tena kujaribu silaha za nyuklia.Hapo jana Korea Kaskazini ilifanya jaribio jingine la aina mpya ya makombora katika tukio ambalo limeshuhudiwa na kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong Un aliyehimiza kuimarishwa kwa uwezo wa ulinzi na nguvu za nyuklia wa nchi yake.