Tukio la maporomoko ya udongo lilitokea katika wilaya ya Kadutu, huko Bukavu jioni ya Jumatatu Aprili 25 na kuua watu wanane, akiwemo mwanamke mjamzito na mwanafunzi, na tisa kujeruhiwa vibaya. Nyumba tano na magari matatu pia yaliharibiwa.
Idadi hii inaweza kuongezeka katika saa zijazo, imesema Hlmashauri ya manispaa ya jiji la Bukavu, katika mkoa wa Kivu Kusini, Mshariki mwa DRC.
Zoezi la utafutaji lnaendelea ili kutoa miili yote ambayo bado imekwama chini ya vifusi.
“Inashukiwa kuwa kuna miili mingine chini ya vifusi. Tunachimba na kuondoa vifusi, kuwazika wafu, kusaidia familia zilizoathirika,” alisema Meshach Bilubi, meya wa mji wa Bukavu.
Anasema sababu ya maporomoko haya ni hasa ujenzi mbaya ambao hauzingatii viwango:
"Sababu, kwanza ni sehemu isiyofaa. Ni kilima cha zaidi ya 70% ya mteremko. Kisha kuna nyumba zilijengwa bila kuzingatia vigezo. Tunajenga nyumba za ghorofa kwenye ardhi ambayo sio imara. Ni lazima pia kutambua kwamba hapa ndipo ufa unapita iliosababisha parokia ya watawa wa kidini kuanguka karibu na Lycée Wima. Wanashutumu mamlaka, lakini mara nyingi familia hizi hazina hati miliki za ardhi,” imelaumu mamlaka ya mji.