Waasi wa Tigray waondoka eneo la Afar

Waasi wa Tigrayan wa TPLF wamejiondoa kabisa kutoka eneo la Afar kaskazini mashariki mwa Ethiopia. Walikuwa wamekalia eneo la kaskazini mwa jimbo hili tangu mwishoni mwa wa Januari, wakitaka kujihami dhidi ya mashambulizi ya serikali ya Ethiopia na mshirika wake, Eritrea.

Dalili inayowezekana ya kupungua kwa kasi kwa mapigano: TPLF sasa inaondoka katika eneo hili, hasa kwa matumaini ya kupata misaada ya kibinadamu.

Ni kupitia jimbo hili la Afar ambapo msaada wa chakula unatakiwa kupitishwa hadi Tigray wenye wakazi milioni sita. Kwa miezi kadhaa, imekuwa karibu imesisitishwa, kwa sababu ya serikali kukataa kuruhusu sehemu kubwa ya misafara kupita, lakini pia kwa sababu ya uvamizi wa kijeshi wa waasi wa Tigray katika sehemu ya kaskazini ya eneo hilo.

"Tumejiondoa kabisa kutoka Afar," msemaji wa  wa kundi la waasi la Tigray People's Liberation Front (TPLF) alisema Jumanne, Aprili 26.

Lakini kulingana na vyanzo kutoka jimbo la  Afar, ilikuwa ni mapigano ya siku chache zilizopita ambayo yalilazimisha waasi wa Tiger kurudi nyuma. Waasi wamejiondoa hasa kutoka kwa barabara ambayo misafara ya kibinadamu inapita na watadumisha uwepo wao kaskazini mwa jimbo la Afar.

Je, kujitoa huku kunamaanisha kuwa makubaliano yamefikiwa kati ya Addis Ababa na waasi wa Tigray? Si lazima, kutokana na taarifa ya hivi punde kwa vyombo vya habari kutoka TPLF. Katika barua kwa Umoja wa Mataifa, waasi walitishia kutumia nguvu tena ikiwa hakutakuwa na mchakato wa amani wa kuaminika utakaofanyika nchini Ethiopia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii