Kampuni kubwa inayotengeneza ndege zisizo na rubani, DJI, inatangaza "kusitishwa" kwa shughuli zake za kibiashara nchini Urusi na Ukraine, na kuwa moja ya kampuni chache za Kichina kuchukua hatua kama hiyo hadharani.
Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Mykhailo Fedorov aliandika barua mwezi uliopita kwa kampuni ya DJI akishutumu jeshi la Urusi kwa kutumia "bidhaa" za kampuni hiyo kuwalenga raia.
Wiki iliyopita, kampuni ya China ilikashifu upotoshaji wa kijeshi wa bidhaa zake. "DJI imewahi tu kutengeneza bidhaa kwa matumizi ya kiraia," ilisema. "DJI daima imekuwa ikipinga kwa dhati majaribio ya kuweka silaha kwenye bidhaa zake" na "imekataa kubinafsisha au kuruhusu marekebisho ambayo yangeruhusu bidhaa zetu kutumika kwa madhumuni ya kijeshi," kampuni hiyo imebaini.
Mshirika wa karibu wa kidiplomasia wa Moscow, Beijing imeaibishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, lakini hadi sasa imekataa kulaani uvamizi huo, na kuyaweka makampuni ya Kichina katika hali ya sintofahamu.