Man City yaipiku Real Madrid katika mechi ya kusisimua ya Ligi ya Mabingwa

Manchester,Manchester City wana uongozi mwembamba wa kuulinda katika mkondo wa pili wa nusu fainali yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid baada ya kushinda mkondo wa kwanza wa kusisimua kwa mabao 4-3 uwanjani Etihad jana usiku. Mabingwa hao wa England huenda wakajutia nafasi walizopoteza dhidi ya mabingwa hao mara 13 wa Ulaya baada ya kuwa kifua mbele mara tatu kwa mabao mawili. Kevin De Bryune, Gabriel Jesus, Phil Foden na Bernado Silva waliwafungia vijana hao wa Pep Guardiola, ambao wangefunga hata mengi zaidi. Lakini mabao mawili ya Karim Benzema na moja la Vinicius Junior yaliipa Madrid matumaini ya kuwa na mpambano mwengine mkali wa Champions League dimbani Santiago Bernabeu Mei 4. Hii leo, Liverpool watawakaribisha Villarreal dimbani Anfield.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii