Korea Kaskazini inajivunia nguvu kubwa ya kijeshi

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskani vimetangaza taifa hilo kupata kile ilichokiita nguvu isiyoweza kushindwa, ambayo ulimwengu hauwezi kuipuuza na hakuna anaweza kuisogelea.Vyombo hivyo vimeongeza kutaja mafanikio hayo kuwa yamepatikana chini ya kiongozi wa taifa hilo Kim Jog Un, hatua ambayo inaonesha dhahiri ushahidi mwingine wa silaha zake za nyuklia, katika kipindi hiki serikali ya Pyongyang ikijiandaa na mapunziko ya kijeshi.Taarifa za shirika la habari la taifa hilo, KCNA zimeorodhesha historia ya mafanikio ya kijeshi ya taifa hilo kuanzia vita vyake dhidi ya Marekani 1950 hadi 1953, makabiliano madogomadogo katika kipindi cha Vita Baridi hadi mwaka 2010.Kesho Jumatatu ni siku ya kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Mapinduzi la Watu wa Korea, na wachunguzi wa kimataifa wanatarajia Korea Kaskazini kufanya gwaride kubwa la kijeshi na ikiwezekana kufanya maonyesho mengine ya silaha zake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii