WHO yasema watoto milioni moja wamechomwa chanjo ya Malaria Afrika

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema mpango wa majaribio wa chanjo ya malaria katika nchi za Kenya, Ghana na Malawi unaendelea vyema. Akizungumza mjini Geneva jana, Katibu Mkuu wa shirika hilo la afya la Umoja wa Mataifa Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema zaidi ya wavulana na wasichana milioni moja wamechomwa chanjo hiyo ya RTS,S tangu mwaka 2019. Tedros ameitaja hatua hiyo kama "mafanikio ya kisayansi" ambayo huenda yakayabadilisha na kuyafanya kuwa mazuri, maisha ya mamilioni ya watu. Inaripotiwa kwamba wafadhili wa kimataifa watatoa dola milioni 155zaidi kwa ajili ya kutolewa kwa huduma hiyo ya chanjo katika nchi zilizo chini ya jangwa la sahara. Asilimia 94 ya maambukizi ya malaria huripotiwa katika nchi hizo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii