Kiungo Mshambuliaji wa Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’ Lambart Sabiyanka amesema anaamini kikosi cha klabu hiyo kitapmbana hadi mwisho ili kuhakikisha wanabaki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Tanzania Prisons ina wakati mgumu katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ikiwa nafasi za chini katika msimamo baada ya kucheza Mechi 19 hadi sasa.
Sabiyanka amesema bado wachezaji wa klabu hiyo wana uhakika wa kuibakisha timu yao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao licha ya kuendeleaa kuwa mkiani mwa msimamo.