Hayo
yamebainishwa na Meneja Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani kutoka
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Maguha Stephano kwenye kampeni
ya uchunguzi wa Saratani iliofanyika mkoani Njombe na kuhudhuriwa na
wananchi 600 huku wengi wao wakiwa ni akina mama.
Amesema
Wanaume walijitokeza walikua 103 sawa na asilimia 17, waliopimwa na
kukutwa na viashiria hivyo vya Saratani ya tezi dume na walipewa rufaa
ya kwenda taasisi ya Saratani ocean road kwa uchunguzi zaid na matibabu.
Kwa
upande wa Wanawake Dkt. Maguha amesema Wanawake waliojitokeza ni 497
sawa na asilimia 83 huku wanaume wakiwa 103 sawa na asilimia 17 na
kufanyiwa vipimo vya magonjwa mbalimbali ya Saratani.
"Wanawake
Saba ambao walifanyiwa uchunguzi wa Saratani ya matiti walikutwa na
uvimbe na wawili walikuwa na viashiria vya Saratani ya matiti".
Pia,
wanawake wengine waliofanyiwa uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi
10 walikutwa na mabadiliko ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi
(precancerous lesions) na walipatiwa tiba (cryotherapy) ili kuzuia
saratani ya mlango wa kizazi na wanawake wawili walikutwa na Saratani ya
mlango wa kizazi na kupewa rufaa kwenda Ocean road.
Kampeni
hiyo ya uchunguzi wa Saratani mkoani Njombe ilianza tarehe 8 mpaka 10
April, 2022 na kutolewa kwa wananchi wote bila malipo.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii