Waziri Nape aongea kuhusu uwekaji wa anwani za Makazi

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema zoezi la uwekaji wa anwani za Makazi limefikia asilimia 68 huku akiitaja mikoa ya Dar es salaam na Tanga kuwa bado haijafanya vizuri kwenye zoezi hilo

Nape ameyasema hayo leo April 11, 2022 wakati akiwa katika uwanja wa ndege jijini Dodoma akijiandaa kuanza safari ya kuzunguka nchi nzima kufanya uhamasishaji wa uwekaji anwani za makazi. Waziri Nape anaanza ziara hiyo Leo mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii