Petro de Luanda ya Angola yaishinda FAP ya Cameroon

Baada ya kushindwa Ijumaa usiku na Zamalek ya Misri, Petro de Luanda ya Angola ilirejea uwanjani Jumamosi na kushinda dhidi ya Forces Armées et Police Basketball- FAP  ya Cameroon kwa jumla ya pointi 73-60.

Baada ya kushindwa Ijumaa usiku na Zamalek ya Misri, Petro de Luanda ya Angola ilirejea uwanjani Jumamosi na kushinda dhidi ya Forces Armées et Police Basketball- FAP ya Cameroon kwa jumla ya pointi 73-60.

Keumoe wa Cameroon alimpasia Byers ambaye aliurudisha kwa Keumoe naye alipachika pointi mbili za kwanza za mchezo huo.

Mabingwa hao wa Angola walijibu wakati Morais alipompasia Gakou ambaye aliweka mpira nyavuni.

Pedro wa Luanda alizidi kupanua uongozi wa timu yake alipofunga pointi mbili na kufanyiwa madhambi.

Domingos wa Petro alimpasia Paulo ambaye alikaribia kikapu lakini mpira wake ulizuiwa na Bidias wa FAP huku Toko akipata mpira wa uliorudi na kumpasia Bidias upande wa pili wa uwanja aliyepachika pointi mbili.

Zikiwa zimesalia dakika 2 kipindi cha kwanza kumalizika, Gonçalves wa Petro alimpasia Moreira aliyeingiza nyavuni kwa mkono mmoja.

Naye Bidias wa Cameroon alijaribu kupunguza uongozi wa Angola wa pointi 9 huku akipachika pointi mbili kwa timu yake.

Gakou wa Petro alimpasia Dundão ambaye alipachika pointi tatu, akiendeleza uongozi wao hadi pointi 10 katika kota ya 3.

Zikiwa chini ya dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika, Joaquim wa Petro alimpasia Gonçalves ambaye alipiga pasi ya haraka kwa Pedro lakini alirudishiwa na kufunga pointi mbili.

Petro wakiwa juu kwa pointi 16 Gonçalves alimpasia Dundão aliyepachika pointi ya masafa marefu na kusukuma uongozi wao hadi pointi 19.

Na walimaliza mchezo huku Petro wakichukua ushindi kwa pointi 13 na kuandikisha ushindi wao wa tatu wa kanda ya Nile huku FAP wakipoteza mchezo kwa mara ya pili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii