Mwendesha Mashkata Mkuu wa Mahakama ya Kimatiafa (ICC), Karim Khan, amesema ataendelea kujaribu kufanikisha upatikanaji wa Urusi katika kujihusisha na uchunguzi wa uhalifu wake wa kivita huko Ukraine.Akizungumza baada ya kuwasili mjini Kyiv, ambapo serikali ya Ukraine imesema matendo maovu yalifanyika dhidi ya binaadamu katika kipindi hiki cha uvamizi wa Urusi, Khan amesema ataendelea kuutafuta upande wa Urusi kwa mara ya tatu.Urusi umezipuuzilia mbali tuhuma za majeshi yake kufanya uhalifu wa kivita tangu iivamie Ukraine Februrari 24 kwa kusema ni habari za uzushi.