BANDARI ya Tanga inatarajiwa kuanza
kupokea Meli za Magari ifikapo Mwezi Mei mwaka huu ambayo yatakuwa
yakipelekwa kuhifadhiwa eneo la Mwambani Jijini Tanga .
Hatua
hiyo inatajwa kwamba itafungua fursa mpya za kiuchumi kwenye Bandari
ambayo kwa sasa inafanyiwa maboresho makubwa ili kuongeza ufanisi katika
utoaji wa huduma zake.
Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa
Bandari ya Tanga Mrisha Masoud wakati wa ziara ya wadau wa Bandari ya
Tanga walipotembelea bandarini baada ya kumalizika kwa kikao chao na
mamlaka hiyo.
Meneja Mrisha alisema eneo la mwambani lina ukubwa
wa hekta 176 sasa kama walivyosema wanatarajia kuhudumia shehena kubwa
kutoka 750,000 mpaka kufikia Milioni 3000,000 hivyo mzigo utakuwa ni
mwingi.
Alisema kutokana na hilo wamependelea eneo hilo
watalitumia kufanya shughuli za nyengine ikiwemo kupakilia mizigo kwenye
makontena na kuweka kontena tupu na shughuli zinazoambatana na shughuli
za kibandari
Hata hivyo aliwaeleza wadau hao kuhusu maboresho
ya Bandari ya Tanga ikiwemo jinsi mradi wa maboresho ulivyo mpaka sasa
awamu zote tatu ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni kuongeza kina kutoka
mita tatu mpaka mita 13 kwenye mlango bahari,sehemu ya kujeuzia meli na
vifaa ambapo iligharimu Bilioni 172.3.
Alisema pia wameona
maboresho ya base mbili zenye urefu mita 450 zilizogharimu Bilioni 256.8
na wameona ahadi iliyolewa na mkandarasi ambapo mpaka mwezi Mei
watakabidhiwa kipande cha mita 150 na itakapofika octoba wakabidhi mita
zote 450.
Hata hivyo alisema kwamba hoja ambazo zimewasilishwa
na wadau kwenye kkao hivho wamezichukua na kwenda kuzifanyia kazi na wao
wametusikiliza kuwaeleza namna maboresho makubwa yaliyofanyika na
kuhaidi kuitumia kwa ajili ya kupitisha shehena zao.
Awali
akzingumza mara baada ya ziara ya wadau hao kwenye Bandari hiyo
kushuhudia maboresho makubwa yaliyofanyika Kaimu Mkurugenzi wa masoko na
Uhusiano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Makao Makuu Nikodemas
Mushi alisema mkutano huo ulikuwa na nia ya kukutana na wadau
wanaohudumiwa na Bandari ya Tanga ambayo inayohudumia mikoa ya kanda ya
kaskazini ikiwemo nchi Jirani Rwanda.
Alisema kupitia mkutano
huo wanaamini watafungua ukurasa mpaya wa kiboshara na lengo lao ni
kuondoa nafasi ya maswali na hoja na changamoto mbalimbali ambazo
hazijaweza kutoka upande mmoja kwenda mwengine.
Kaimu Mkurugenzi
huyo wa Masoko na Uhusiano alisema wadau wametoa maoni huku akieleza
kwamba Meneja wa Tanga na timu yake wamesikia na wamejipanga tayari
kuanza kuzifanyia kazimara moja,.
Alisema na suala ambalo
linawahusu makao makuu watalibeba na kulipeleka huku ili yaweze
kufanyiwa maamuzi na huo ni mkakati wa kimasoko