WAKAZI wa Jimbo la Mpendae Visiwani
Zanzibar wamepata faraja Kwa familia ya Marehem Salim turkey Kwa
kuendeleza yale mazuri kwa wananchi wake hususani kuwakumbuka watu wenye
uhitaji katika kipindi cha Mfungo wa Ramadhani.
Akizungumza na
Michuzi Tv Mtoto wa Marehem Salim turkey, ambae ni Mbunge wa jimbo hilo
Toufiq Salim amesema mara Kwa mara wakati wa Mwezi wa Ramadhani Marehemu
alikua akiwakumbuka watu wenye uhitaji na kugawana nao kidogo
anachopata.
"Wananchi walijua hatutaweza kuendelea na utaratibu
huo lakini kutokana na misingi mizuri aliyoacha mpendwa wetu, jukumu
hilo tumelibeba sisi familia yake na Leo tumegawa Mkono wa futari Kwa
takribani watu 4000 katika Jimbo la Mpendae hapa Visiwani Zanzibar."
Aidha
Miongoni mwa vitu vilivyogaiwa Kwa watu hao ni pamoja na vyakula
mbalimbali ikiwemo Mchele, Maharage,mafuta, Sukari,unga pamoja na pesa.