EU kutumia diplomasia ya chakula kukabiliana na kupanda bei ya ngano

BRUSSELS Umoja wa Ulaya unalenga kukabiliana na kupanda kwa bei ya ngano na mbolea kwa kujihusisha na kile ulichokitaja kuwa diplomasia ya chakula. Kupanda kwa bei za bidhaa kunatarajiwa kusababisha uhaba wa chakula katika ukanda wa Balkani, Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati. Mwanadiplomasia mmoja wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa ukosefu wa chakula husababisha chuki katika nchi zilizo hatarini katika maeneo hayo. Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema wiki iliyopita kwamba vikwazo vya Magharibi vimechochea mzozo wa chakula duniani. Nchi kama vile Misri na Lebanon zinategemea sana uagizaji wa ngano na mbolea kutoka Ukraine na Urusi. Umoja wa Ulaya utatangaza mipango mipya kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii