Umoja wa MataifaRipoti ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa ugonjwa wa Covid-19 ulisababisha zaidi ya watu milioni 77 kutumbukia katika umaskini uliokithiri mwaka jana huku nchi nyingi zinazoendelea zikishindwa kujinasua kutokana na ulipaji wa madeni. Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed amesema vita nchini Ukraine vitazidisha changamoto hiyo kutokana na kupanda kwa bei ya nishati na bidhaa nyingine, mfumuko wa bei, ukuaji mdogo na kuongezeka kwa wasiwasi katika masoko ya fedha. Ripoti hiyo inapendekeza kuharakisha msamaha wa madeni na kupanua ustahiki kwa nchi zenye deni kubwa za kipato cha kati, kuoanisha mfumo wa kimataifa wa kodi ili kushughulikia masuala kama vile ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa chanjo ya virusi vya corona.