Na katika michezoBayern Munich wametupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Champions League baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Villarreal. Katika mechi ya kwanza Villarreal ilikuwa imeshinda bao 1-0 dhidi ya Bayern. Bao la Samuel Chukwueze katika dakika ya 88 liliipa ushindi Villarreal katika mchezo wa pili wa robo fainali. Klabu hiyo imetinga nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu 2006. Katika mchezo mwingine Real Madrid wamesonga hatua ya nusu fainali baada ya kuitandika Chelsea ambaye alikuwa ndio anashikilia taji katika dakika za nyongeza. Mechi nyingine zitakazopigwa leo ni kati ya Atletico Madrid na Manchester City wakati Liverpool ikivaana na Benfica.