The HagueShirika la kuzuia kuenea kwa silaha za kemikali duniani OPCW limesema kuwa lina wasiwasi na ripoti za matumizi ya silaha za kemikali katika mji uliozingirwa wa Mariupol nchini Ukraine. Ripoti hizo zilianza kusambaa tangu siku ya Jumatatu kwamba ndege ya Urusi isiyokuwa na rubani ilidondosha dutu yenye sumu dhidi ya vikosi vya Ukraine na raia, katika mji huo wa bandari. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, amesema wanazo taarifa za kuaminika kwamba Urusi inaweza kutumia silaha hizo katika mashambulizi yake ya kuudhibiti mji wa Mariupol. Mara ya mwisho silaha hizo kutumiwa ilikuwa ni katika mzozo wa vita vya Syria vilivyozuka mwaka 2011.