Shirika la kimataifa la kutetea usawa wa kijinsia na haki za wanawake limetangaza kumteuwa dkt Maliha Khan, kuwa rais wa shirika hilo.
Kabla ya kuteuliwa kwake daktari Khan, alikuwa mkuu wa mipango, katika taasisi ya Malala, Khan akimrithi Kathaleen Sherwin, ambaye amekuwa kaimu rais na mkurugezi wa Women Deliver tangu Juni mwaka 2020.
Kibarua kinachomsubiri Khan kwa sasa ni kuhakikisha utekelezaji wa ruwaza ya shirika hilo ya mwaka 2021 – 2025, kuhakikisha Women Deliver linazidi kupingania haki za wanawake.
'Nimefurahi sana kuteuliwa kuongoza shirika hii kama rais na mkurugezi mkuu, mimi ni mwanaharakati ambaye nimekuwa kwa muda nikipigania haki za wanawake na wasichana, na kuhakikisha utekelezaji wa haki na sheria za wanawake zinatekelezwa’ amesema Maliha Khan' baada ya kukubali uteuzi wake.
Kathaleen Sherwin, ambaye amekuwa kaimu rais wa shirika hilo, amejukumiwa kutoa ushauri wa usimazi kwa Khan hadi Juni mwaka huu, akisema ana imani na uongozi wake.
Tayari shirka hilo limetangaza kuandaa kongamano lake nchini Rwanda, ikiwa ni mara kwanza kabisa mkutano wake kuandaliwa barani Africa, kati ya July 17 hadi 20 mwaka ujao, wajumbe zaidi ya 6,000 wakitarajiwa kuhudhuria mkutano huo.