RASIMMAFUTA YAPANDA BEI

Wakati bei ya Mafuta yanayotumika kwenye vyombo vya moto ikitangazwa kupanda mara dufu, wananchi wa jiji la Dar es salaam wameonekana usiku wa kuamkia Leo wakipanga foleni katika vituo vya Mafuta ili kujikwamua kujaza Mafuta kwenye vyombo vyao kabla ya bei hiyo kupanda.

Kwa sasa watumiaji wa nishati hiyo watalazimika kufunga mkanda kutokana na bei za bidhaa mbalimbali za vyakula pia kuendelea kupanda hasa wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani zikiwemo pia bei za Mafuta ya kula.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni alisema hadharani kuwa kila enen la kiuchumi lipatanda bei kuaniza mafuta, nauli na vyakula vyote.

“Tumeanza kusikia minong’ono huko ‘maisha yanakuwa magumu sijui kila kitu kinapanda bei hao Viongozi wetu tulionao hawana baraka hawana nini’, si baraka ya Kiongozi ni hali ya Ulimwengu inavyokwenda, mafuta yanapanda bei Duniani na vitu vitapanda bei,” alisema Rais Samia.

Hata hivyo, vita vya Russia na Ukraine ambavyo vimedumu kwa zaidi ya mwezi sasa navyo vinatajwa kupandisha bei ya nishati hiyo kwenye soko la dunia, ikiwa Russia ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Jumanne Aprili 5, 2022 Mkurugenzi wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Gerald Maganga amesema kuanzia Jumatano, Aprili 6, 2022 bei mpya ya petrol kwa mafuta yanayopokelewa kupitia Bandari ya Dar es salaam itakuwa Sh2,861 kutoka Sh 2,540 ikiwa ni ongezeko la Sh321.

Kwa upande wa dizeli bei mpya itakuwa Sh2,692 kutoka Sh2,403 ya sasa ikiwa ni ongezeko la Sh289. Bei ya mafuta ya taa itapanda kutoka Sh2,208 hadi Sh2,682 ikiwa ni wastani wa Sh474.

Maganga amesema mafuta ambayo yatapitia Bandari ya Tanga, bei ya petrol itakuwa Sh2,848 kutoka Sh2,563 ikiwa ni ongezeko la Sh285, kwa upande wa dizeli bei itaongezeka kutoka Sh2,484 hadi Sh2,779 ikiwa ni ongezeko la Sh295 kwa lita moja.

Mafuta ambayo yatapokewa kupitia Bandari ya Mtwara bei ya petrol kwa lita moja itakuwa Sh2,678 kutoka Sh2,577 ikiwa ni ongezeko la Sh100, Bei ya dizeli kwa lita moja itakuwa Sh2,811 kutoka Sh2,530 ikiwa ongezeko la Sh281.

Hata hivyo, Maganga amesema kuwa bei hizo zimejumuisha tozo ya Sh100 ambayo Serikali ilitangaza kuiondoa mwezi Machi, 2022 kabla ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kuirejesha akisema utaribu wa kuindoa haukufuatwa kwa kuwa fedha hiyo ilishapangiwa bajeti.

Nchini Kenya, Rais Uhuru Kenyatta alitia saini sheria itakayowezesha kampuni za kusambaza mafuta kupata jumla ya KSh 34.4 bilioni kutoka kwenye bajeti ya ziada zilizotengewa mpango wa serikali kuthibiti bei ya mafuta.

Kulingana na Ikulu ya Kenya, Bajeti mpya ya Nyongeza iliyotiwa saini ni fedha za hazina na kando na kutoa ruzuku kwa bei ya mafuta, fedha hizo pia zitashughulikia changamoto zinazohusiana na ukame na maandalizi ya uchaguzi.

Wakenya walifurahia baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini sheria ya kutoa fedha za kumaliza tatizo la uhaba wa mafuta nchini baada ya video ya wahudumu wa petroli kuonekana wakisherehekea kuwasili kwa lori la Mafuta huku wakiimba: “Yote yawezekana kwa imani.”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii