Umoja wa Mataifa waomba uchunguzi huru wa madai ya mauaji ya kimbari nchini Mali.

Mali imesema jana kwamba wachunguzi wa kijeshi wameanza kuchunguza matukio yaliyotokea kwenye kijiji cha Moura kunakodaiwa vikosi vyake na vya kigeni vilifanya mauaji ya kimbari. Awali mtaalamu wa shirika la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa Alioune Tine alitoa mwito wa uchunguzi huru wa madai hayo katika eneo hilo linalokabiliwa na mzozo na kuziomba mamlaka za Mali kuruhusu ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Minusma kufanya uchunguzi huo. Jeshi la Mali lilitangaza Aprili Mosi kwamba limewaua wanamgambo 203 katika kijiji hicho mwishoni mwa mwezi Machi lakini mapema wiki hii Shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch lilisema jeshi hilo liliwaua raia 300 katika operesheni hizo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii