Polisi wa mji wa Sacramento katika jimbo la California nchini Marekani imesema imemkamata mtu anayeshukiwa kufanya shambulizi la bunduki lililouwa watu sita na kuwajeruhi wengine 12 usiku wa Jumapili. Mshukiwa huyo ametambulishwa kama Dandre Martin mwenye umri wa miaka 26 anashikiliwa kwa mashitaka ya kushambulia watu na kumiliki bunduki kinyume na sheria. Mashambulizi hayo yalitokea saa za aljajir wakati vilabu vilipokuwa vinafunga milango katika mtaa ambako kuna uwanja wa timu ya mpira wa kikapu ya Sacramento Kings. Baada ya mkasa huo polisi ilifanya upekuzi katika majengo matatu, ambapo ilikamata bunduki na risasi zipatazo 100.