Watu 150 hawajulikani waliko Nigeria baada ya treni yao kushambuliwa

Watu wasiojulikana waliojihami kwa bunduki wameishambulia treni kwa viripuzi kaskazini magharibi mwa Nigeria, na hadi sasa watu 150 waliokuwa wakisafiri kwa treni hiyo hawajulikani walipo. Wapatao wanane waliuawa katika shambulizi hilo lililotokea tarehe 28 Machi. Washambuliaji hao kwanza waliripuwa bomu kwenye reli ilipokuwa inapita treni hiyo, na kisha wakaanza kuwamiminia risasi wasafiri waliokuwa wakitoka mjini Abuja kwenda Kaduna. Rais wa Nigeria amesema wakati hayo yakitokea, baadhi ya wasafiri walikuwa tayari wametekwa nyara. Hilo ni tukio la hivi karibuni kabisa, katika mfululizo wa mengine yanayofanywa na magenge ya wahalifu katika eneo hilo. Magenge hayo yanashambulia vijiji na miji, na kuwachukuwa mateka watu wengi, ambao baadaye wanatoza fidia ili wawaachie huru

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii