Eu yaitaka China kutoisaidia Urusi katika vita vya Ukraine

Viongozi wa Umoja wa Ulaya na China wamekutana leo kwa mara ya kwanza katika miaka miwili, huku Brussels ikiishinikiza Beijing kutoa uhakikisho kwamba haitopatia Urusi silaha wala kuisadia Moscow kukwepa vikwazo vya magharibi kuhusiana na uvamizi wake nchini Ukraine. Marais wa Baraza la Ulaya na Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Charles Michel na Ursula von der Leyen, pamoja na mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo Josep Borrell, wameanza mazungumzo na waziri mkuu wa China Li Keqiang, na wanatarajiwa baadae leo kuzungumza na rais wa China Xi Jinping. Afisa wa Umoja wa Ulaya amesema msimamo wa China kuelekea Urusi ndiyo swali kuu leo, huku mwingine akibainisha kuwa robo ya biashara ya kimataifa ya China ilikuwa na kanda hiyo na Marekani mwaka uliopita, ikilinganishwa na asilimia 2.4 iliyofanya na Urusi. Mkutano huo unaofanyika kila mwaka, haukufanyika mwaka jana baada ya kuzuka mzozo kati ya Umoja wa Ulaya na China kuhusaiana na namna nchi hiyo inavyowatendea watu wa jamii ya wachache ya Uighur.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii