Warusi waondoka Chernobyl wakati mapigano yakiendelea kwingineko

Wanajeshi wa Urusi wamekabidhi udhibiti wa kiwanda cha nyuklia cha Chernobyl kwa Waukraine na kuondoka eneo hilo lililochafuliwa na mionzi kwa kiasi kikubwa mapema leo. Maafisa wa Ukraine wamesema Warusi wamekirudisha kutokana na kuathiriwa na mionzi, ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja baada ya kukichukua, wakati mapigano yakipamba moto kwenye viunga vya Kyiv na maeneo mengine. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema kuondoka kwa Urusi katika maeneo ya kaskazini na katikati mwa nchi ni mbinu ya kijeshi na kuwa askari wanajikusanya kwa ajili ya kufanya mashambulizi mapya makali kusini mashariki. Wakati huo huo, msafara wa mabasi 45 ulielekea Mariupol katika jaribio jingine la kuwahamisha watu kutoka mji huo wa bandari uliozingirwa baada ya jeshi la Urusi kukubali kusitisha kwa muda mapigano katika eneo hilo. Lakini kwa mujibu wa serikali ya Ukraine, askari wa Urusi waliyazuia mabasi hayo, na watu 631 pekee waliweza kuondoak mini humo katika magari ya kibinafsi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii