Jeshi la DRC ladai kuwakamata wanajeshi wawili wa Rwanda

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inathibitisha na kushikilia kuwa Rwanda inaunga mkono waasi wa M23, vuguvugu ambalo lilishindwa miaka kumi iliyopita lakini limeibuka tena katika miezi ya hivi karibuni.

Kundi hili linashutumu ukosefu wa maendeleo katika mchakato wa kurejea kwa wapiganaji wake katika ardhi ya Kongo. Kumekuwa na mapigano tangu mwisho wa mwaka 2021, lakini yamekuwa yamepooza na kuwa mapigano ya nguvu kwa siku chache sasa katika eneo la Rutshuru, kaskazini mwa Goma, huko Kivu Kaskazini. Mnamo Machi 28, mapigano mapya yalitokea, M23 walishambulia maeneo ya jeshi la Kongo. FARDC wanadai kuwakamata wanajeshi wawili wa Rwanda katika operesheni ya kujibu mashambulizi ya waasi.

"Wakati wa mashambulizi haya, anasema Luteni Jenerali Brigedia Sylvain Ekenge, naibu msemaji wa FARDC na msemaji wa gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini, FARDC iliwakamata wanajeshi wawili wa Rwanda. "

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii