Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya gari aina ya fuso walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika eneo la barabara ya Soni/Mombo wilayani Lushoto mkoani humo.
Akizungumza na Jembe FM leo Jumanne Machi 29, 2022 Kamanda Safia amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi.