Mchungaji mmoja amewashauri wanaume kutooa wasichana wavivu. Mahubiri yake yalikuwa yanawalenga warembo ambao huomba nauli wakienda deti.
Pasta wa Kike Azua Gumzo Akisema Warembo Wanaomba "Fare" ni Maskini
Kulingana naye, wanaume hawafai kuoa wasichana wanaoomba nauli kwa sababu ni ishara kuwa warembo hao ni maskini.
Pasta huyo aliangazia dhana kwamba ni mwanamume ndiye anapaswa kuwajibikia usafiri wa mpenzi wake.
Alidai kwamba badala yake mrembo pia anaweza kumchukua mwanamume na gari lake na kumpeleka kwenye mgahawa.
"Usioe msichana mvivu. Msichana ambaye atakuomba pesa za usafiri. Ushauri wanaokupa, kwamba mwanaume ndiye anapaswa kutoa nauli ni ishara kwamba mrembo unayemchumbia au unayemvutia ni masikini.Kwani unampaje mtu ambaye tayari aliendesha gari lake huko nauli. Yeye ndiye anatakiwa kukuchukua na kukupeleka kwenye mgahawa. Unatafuta wasichana unaotaka kutoa N2k," alisema.