Mashambulizi mawili kwa mpigo yauwa watu 48 Somalia

Kiongozi wa jimbo la Hirshabelle, Ali Gudlawe Hussein, amesema idadi ya waliokufa kutokana na mashambulizi mawili yalitokea katika karibu kipindi kimoja huko katikati ya Somalia imeongezeka na kufikia watu 48.Wanamambo wa kundi la A-Shabaab wamedai kuhusika na shambulizi hilo ambalo pia limesbabisha watu 108 kujeruhiwa. Limesema lilikuwa likiwalenga polisi, ikiwa kabla ya uchaguzi.Shambulio la kwanza lilitokea Jumatano la kujitoa muhanga katika wilaya ya Beledweyne, na kusababisha kifo cha mbunge Amina Mohamed Abdi na walinzi wake wakati akifanya kampeni ya kuchaguliwa tena.Kundi lenye mfungamano la Al-Qaeda mara nyingi limekuwa likiwalenga raia, wanajeshi na maeneo ya serikali mjini Mogadishu na nje ya jiji hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii