Zelensky ahimiza kufanyika maandamano kimataifa kupinga uvamizi wa Urusi

Kyiv, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa watu duniani kote kuandamana barabarani kama hatua ya kupinga uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Katika ujumbe alioutoa kuelekea mkesha wa kumbukumbu ya mwezi mmoja wa uvamizi wa Urusi, Zelensky amewataka watu duniani kote kusimama imara dhidi ya Urusi na kupinga vita hivyo. Rais huyo wa Ukraine pia ametoa wito kwa muungano wa jeshi la kujihami la NATO kuipa msaada Ukraine ikiwemo wa silaha ili kupambana na wanajeshi wa Urusi. Mamia ya watu wameuawa, na mamia ya wengine wamejeruhiwa huku zaidi ya raia milioni 3 wa Ukraine wakiimbia nchi yao na kutafuta hifadhi katika mataifa jirani. Urusi iliivamia jirani yake Ukraine mnamo Februari 24 kwa lengo la kuizuia nchi hiyo kuelekea Umoja wa Ulaya na kujiunga na NATO.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii