Zaidi ya wanajeshi 10 wauawa katika shambulizi la Burkina Faso

Zaidi ya wanajeshi 10 wameuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi katika eneo la mashariki mwa Burkina Faso, duru za kijeshi zimesema.

Ilifuatia shambulio la Jumapili dhidi ya kikosi cha askari wa doria na usalama huko Natiaboni, mji wa mashambani katika eneo ambalo limekuwa likilengwa mara kwa mara na washambuliaji.

Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso ilichukua mamlaka mwezi Januari na kumuondoa madarakani Rais Roch Kaboré, ikimlaumu kwa kushindwa kukabiliana na waasi wa kijihadi.

Ghasia hizo tangu mwaka 2015 zimesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na kuwalazimisha mamilioni kukimbia makazi yao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii