Ndege ya shirika la ndege la China Eastern Airlines aina ya Boeing 737 iliyokuwa imebeba watu 132 imeanguka katika mkoa wa Guangxi, vyombo vya habari vya serikali ya China vinaripoti.
Idadi ya waliofariki bado haijajulikana.
Ajali hiyo, katika eneo la milimani, ilisababisha moto msituni, vyombo vya habari vya serikali vinaripoti.
Ndege ya MU5735 ilipangwa kuondoka Kunming saa 13:15 na ilikuwa njiani kuelekea Guangzhou.