Urusi yatekeleza shambulio baya la bomu kwenye kituo cha biashara Kyiv

Wanajeshi wa Urusi bado wanajaribu kuzingira mji mkuu wa Ukraine, kyiv, ambapo shambulio la bomu liliua takriban watu wanane usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.

 Kulingana na msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, jeshi la Urusi liko katikati mwa jiji la Mariupol ambapo limependeza kwa mamlaka ya Ukraine kuweka chini silaha, bila mafanikio. Huko Mykolaiv, mashambulizi ya anga yanaendelea kupishana kwa mwendo wa haraka.

 Urusi inadai kuwa imetumia makombora ya hypersonic tangu Ijumaa. Makombora haya yanaweza kuruka kwa karibu kilomita 12,000 kwa saa na kutangaza kwenda mbali kilomita 2,000 hadi 3,000.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Urusi kuzingira bandari ya Mariupol ni "ugaidi ambao utakumbukwa kwa karne nyingi". Mbele ya Bunge la Israel, Knesset, aliiomba Israel "kufanya chaguo" kwa kuunga mkono Ukraine dhidi ya Urusi.

Watu milioni kumi wamekimbia makazi yao nchini Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa jeshi la Urusi mnamo Februari 24, kulingana na Umoja wa Mataifa. Kati ya jumla ya idadi hiyo, zaidi ya wakimbizi milioni 3.3 wameondoka nchini. Takriban raia 902 wameuawa na 1,459 wamejeruhiwa nchini Ukraine, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Haki za Binadamu. imebaini siku ya Jumapili. Kwa kuwa takwimu hizi ni ngumu kuthibitisha, Umoja wa Mataifa unabaini kwamba idadi hii inayotolewa kila siku pengine ni iko chini sana kuliko hali halisi ya mambo.

Vita vililazimisha shule na vyuo kufungwa. Wakati wa wiki mbili za kwanza za vita, serikali ilitangaza likizo, lakini migogoro inaendelea na baadhi ya walimu wanajaribu kuwasiliana na wanafunzi wao na kujipanga kwa kuweka visomo mtandaoni,

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii